Kero: karai kuwa beseni
***************************
kwetu ni injili ya kujichubua
kwa kwenda mbele ni kujikoboa,
ila, madhila hutufika, maji yazidipo unga,
ya ngozi kunadiwa, na gamba la nyoka
kuvulia utawala.
Eti tupinkele huleta njuru na mvua,
na sio kelele za kuamia kweleakwelea!
ndiposa ufisadi huu n’kaubatiza chuburexia.
Hata kama n’gombe mla nyasi
aweza kutoa kivazi cha harusi?
Je, ni iweje cha kutindikwa
kwa jani la mchikichi,
kitoke na rangi ya chanikiwiti?
~ © Dr Morice, 2009.